cd News Post / Tanzania Horticultural Association

News Post

Home /News Room/News Post

FURSA YA MAFUNZO

Image
Posted on 6th Mar | 2019

FURSA YA MAFUNZO KWA WADAU WA PARACHICHI NA VIUNGO. Tanzania Horticultural Association(TAHA) ambayo ni taasisi inayosimamia wadau wa matunda, mbogamboga na viuongo, Mamlaka ya biashara tanzania (TANTRADE), kwa kushirikiana na kituo cha biashara ya kimataifa (ITC) chini ya ufadhili wa umoja wa ulaya EU unatekeleza mradi wenye lengo la kuboresha masoko ili kuongeza mauzo ya nje ya nchi(MARKUP). Tunapenda kuwa taarifu wazalishaji na wafanya biashgara wa kitanzania wadogo na wa kati(SME’s) wanaojishughulisha na mazao ya PARACHICHI na VIUNGO (spices) kuwa kutakuwa na mafunzo ya siku tatu ya kuandaa mkakati wa kuuza bidhaa hizo nje ya nchi mafunzo hayo yatalenga katika kusimamia ushindani wa biashara, kuandaa mkakati wa kuuza nje, kufanya miamala ya kuuza nje na kuandaa mpango wa biashara wa kuuza nje ya nchi. VIGEZO VYA KUSHIRIKI MAFUNZO HAYA NI KAMA IFUATAVYO. 1. Kampuni ndogo na za kati zinazojishughulisha na uzalishaji au biashara ya parachichi na viungo. 2. Kampuni yenye uzoefu wa kuuza bidhaa hizo nje ya nchi au inatamani kuuza nje ya nchi 3. Kampuni iwe na mifumo ya usimamizi na uendeshaji wa biashara 4. Kampuni iwe tayari kuboresha mifumo ya uendeshaji wa biashara 5. Utayari wa kuandaa mipango biashara ya kuuza nje ya nchi na kukamilisha majukumu utakayopangiwa ndani ya muda uliyokubaliwa 6. Utayari wa kutoa na kushirikisha taarifa za biashara na kutekeleza mapendekezo ya mikakati ya kuuza nje ya nchi yatakayotolewa 7. Kampuni iwe na mfumo pamoja na teknolojia ya uzalishaji 8. Kampuni iwe tayari inafanya biashara katika soko la ndani ya nchi 9. Kampuni iwe na wanunuzi wengi katika soko la ndani na nje ya nchi au iwe tayari kutanua wigo wa biashara na kuongeza wateja. Ili kushiriki tafadhali wasiliana na 0763 718849 au tuma email kwenda eric.mwesigwa@taha.or.tz Au tembelea tovuti yetu ya; www.taha.or.tz kwa maelekezo Zaidi na kupata fomu ya usajili. Mwisho wa kujisajili ni tarehe 15 machi 2019.

You might also Like